Kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kinafanya semina kwa watumishi wake kwa lengo la kuwajengea uwezo walimu wote wa shule za Al-Ameed.
Mhadhiri wa warsha ya kwanza alikua ni Ustadh Falahu Hassan Juma, ameongelea ratiba za masomo na kujenga tabia ya usomaji kwa walimu.
Semina hizi zinalenga kuboresha uwezo wa walimu wa shule za Al-Ameed na kutumia vizuri vipaji vyao.
Tambua kuwa semina huwa na mada tofauti kulingana na ratiba za walimu.
Kumbuka kuwa kitengo cha malezi na elimu ya juu huendesha semina, warsha na mashindano ya kielimu kwa lengo la kujenga uwezo wa watumishi wake.