Hafla ya watoto wa mashahidi wa fatwa tukufu walioshiriki kwenye mradi wa semina za Qur’ani

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tukufu chini ya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya, imefanya hafla ya wototo wa mashahidi wa fatwa tukufu ya kujilinda walioshiriki kwenye mradi wa semina za majira ya joto, sambamba na maadhimisho ambayo hufanywa kila mwaka ya fatwa hiyo.

Rais wa Majmaa ya Qur’ani Dokta Mushtaq Abbasi Muan ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kufanya maadhimisho kuna umuhimu mkubwa kwani hubakiza kumbukumbu katika akili za watu”.

Akaongeza kuwa: “Kupitia mradi huu mtukufu wa semina za Qur’ani katika majira ya joto, tunawakumbusha watoto hawa misingi muhimu aliyotuusia Mtume (s.a.w.w) nayo, kupenda taifa ni miongoni mwa Imani. Leo tumewakusanya watoto na kuwafundisha kuwa, kufa shahidi kwa ajili ya taifa lako ni sifa kubwa sana kwa raia mwema”.

Akabainisha kuwa: “Tumekusanya watoto walioshiriki kwenye semina pamoja na rafiki zao waliofiwa na wazazi wao kwa ajili ya kulinda taifa hili, tumewafanyia hafla sambamba na kuita madarasa waliyokua wanasomea kwa majina wa wazawi wao mashahidi, ili kuwafundisha kuwa kulinda taifa na kuuawa katika swala hilo ni utukufu ambao kila mmoja anatakiwa awe nao”.

Kumbuka kuwa hafla hiyo imehudhuriwa na mkuu wa Maahadi ya Qur’ani Shekhe Jawadi Nasrawi na viongozi wengine, ndani ya majengo ya Al-Ameed, kulikua na ujumbe wa Rais wa Majmaa ya Qur’ani na kaswida iliyotaja ushujaa wa mashahidi na msimamo wao iliyoimbwa na Muhammad Amiir
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: