Idara ya Tablighi chini ya kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imehitimisha semina ya kumi na tano iliyodumu kwa muda wa siku kumi na tato.
Kiongozi wa idara Sayyid Muhammad Abdullahi Mussawi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Washiriki wa semina hiyo ni watumishi wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), chini ya utaratibu maalum, semina inalenga kuongeza elimu ya Dini kwa watumishi na kuboresha utoaji wa huduma zao kwa mazuwaru”.
Akaongeza kuwa: “Kila semina inayofanywa huongelea mambo mbalimbali yanayo lenga kuwajenga watumishi kwa ujumla”.
Akabainisha kuwa: “Kutokana na ukubwa wa muitikio wa watumishi wetu katika kushiriki kwenye semina hizi, tumekusudia kupanua wigo sambamba na kutoa mitihani kila mwisho wa semina, kwa ajili ya kutambua alichofaidika mshiriki pamoja na kuwapa vyeti vya ushiriki”.
Akaendelea kusema: “Tunatarajia kuwa na watumishi bora kupitia semina hizi, wanafundishwa mambo ya Dini, Fiqhi, Aqida na mambo ambayo kila mtu anayahitaji, tunaamini wataendelea kunufaika na kujiendeleza zaidi”.
Tambua kuwa semina hizi ni sehemu ya harakati za idara ya Tablighi, zimeanza siku nyingi na bado tunaendelea kuwajenga watumishi wetu watukufu.