Kuendelea kwa semina za program ya (Katika kila nyumba muokozi)

Maoni katika picha
Wataalamu wa Alkafeel wanaendelea kutoa semina za uokozi chini ya kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu, kupitia program ya (Katika kila nyumba muokozi), kwa watumishi wa vitengo vya Atabatu Abbasiyya tukufu.

Mkufunzi wa semina amesema: “Ni muhimu kueneza utamaduni wa utoaji huduma ya kwanza kwa kiwango cha juu katika jamii, na kutambua namna ya kupambana na majanga kwa ujumla”.

Akaongeza: “Semina inamada tofauti, miongoni mwake ni: Namna ya kupambana na matatizo ya moyo kwa wazee na watoto”.

Akaendelea kusema: “Semina hii inalenga watumishi wa vitengo vinavyotoa huduma moja kwa moja kwa mazuwaru, kuna zamu mbili ya ashubuhi na jioni, kila semina inadumu kwa muda wa siku mbili, wanasoma saa (5) kwa siku”.

Akafafanua kuwa: “Wanafundishwa kwa nadhariyya na vitendo, kila kipindi kinawashiriki (10) ilikurahisisha kuwapitia mmoja mmoja na kuangalia walichopata kwenye semina”.

Kumbuka kuwa kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kinaendelea kuratibu warsha na semina za kielimu, zinazolenga kuendeleza watumishi wa Ataba tukufu, katika nyanja tofauti.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: