Maahadi ya Qur’ani tawi la wanawake katika mkoa wa Dhiqaar imefungua semina tatu mpya

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tawi la wanawake/ katika mkoa wa Dhiqaar chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, imefungua semina tatu mpya za usomaji wa Qur’ani na hukumu za tajwidi.

Kiongozi wa tawi bibi Maha Abbasi amesema: “Tumefungua semina tatu za Qur’ani zikiwa na wanafunzi (50) kutoka maeneo tofauti ndani ya mkoa wa Dhiqaar”. Akaongeza kuwa “Wanafundishwa usomaji sahihi wa Qur’ani na hukumu za tajwidi”.

Akabainisha kuwa: “Maahadi imepata muitikio mkubwa kutoka kwa wanawake wa mkoa wa Dhiqaar, sambamba na umuhimu wa pekee unao onyeshwa na kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu kwenye miradi hii ya Qur’ani”.

Kumbuka kuwa Maahadi ya Qur’ani tawi la wanawake chini ya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya, inafanya kazi ya kuandaa kizazi cha wanawake wasomi wa Qur’ani
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: