Mashindano ya Qur’ani kwa nchi tano za Afrika kwa kundi la watoto na vijana

Maoni katika picha
Kituo cha Dirasaat-Afriqiyya chini ya kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kilifanya majaribio ya usomaji wa Qur’ani kwa watoto na vijana kutoka nchi tano za Afrika ambazo ni (Mauritaniya – Senegali – Naija – Mali na Tanzania).

Mkuu wa kituo Shekhe Saadi Sataar Shimri amesema: “Shindano lilifanywa kwa njia ya mtandao katika mwezi wa Ramadhani, kwa lengo la kuhamasisha watoto na vijana wa Afrika kuhifadhi sura fupi fupi ndani ya Qur’ani tukufu

Akaongeza kuwa: “Baada ya kumaliza kipindi kilichopangwa, hivi sasa kwa kushirikiana na Maahadi ya Qur’ani katika mji wa Najafu chini ya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya, tumeanza kufanya mashindamo rasmi ya usomaji na hukumu za tajwidi”.

Akabainisha kuwa: “Shindano linawashiriki (150) wenye umri wa miaka (6 – 15) kutoka nchi tano za Afrika, wako makundi matano kulingana na idadi ya nchi washiriki, kila kundi linawashindani (30), baada ya kumaliza kuwasikiliza tutatangaza majina ya washindi pamoja na kutoa zawadi na vyeti vya ushiriki”.

Kumbuka kuwa kituo cha Dirasaat-Afriqiyya kinaemdelea kuratibu harakati mbalimbali katika bara la Afrika, ikiwa ni pamoja na mashindano haya ambayo yanasaidia kuwepo kwa mawasiliano na nchi za Afrika, sambamba na kusaidia kupatikana kwa watoto na vijana mahafidhu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: