Zaidi ya wanafunzi 1300 wanashiriki kwenye mradi wa semina za majira ya joto katika mkoa wa Muthanna

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tukufu chini ya Majmaa ya Qur’ani, inafanya vikao vya usomaji wa Qur’ani katika majira ya joto mkoani Muthanna.

Idadi ya wanafunzi wanaoshiriki kwenye mradi huo imefika (1349) kutoka maeneo tofauti ndani ya mkoa huo.

Walimu wapo (28) wanafundisha usomaji wa kitabu cha Mwenyezi Mungu mtukufu na kukihifadhi, sambamba na Aqida, Fiqhi, Akhlaq na Sira, mradi unatarajiwa kuendelea hadi baada ya sikukuu ya Iddil-Adh-ha.

Tambua kuwa Maahadi ya Qur’ani na matawi yake imepokea wanafunzi (25000) katika mkoa mtukufu wa Karbala na mikoa mingine.

Kumbuka kuwa Maahadi ya Qur’ani na matawi yake ni sehemu ya kituo cha Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya tukufu, inajukumu la kufundisha Qur’ani na kuchangia katika kutengeneza jamii ya wasomi wa Qur’ani kwenye kila sekta.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: