Jopo la madaktari limefanikiwa kutibu goti la mgonjwa mwenye umri wa zaidi ya miaka arubaini

Maoni katika picha
Jopo la madaktari katika hospitali ya Alkafeel, limefanikiwa kufanya upasuaji wa maungio ya goti la mwanaume aliyejeruhiwa miaka mingi iliyopita, daktari amesisitiza umuhimu wa kufanya vipimo mapema.

Daktari bingwa wa upasuaji wa viungo Dokta Ahmadi Suleimani amesema: “Tumefanya upasuaji wa goti kwa mgonjwa mwenye umri wa miaka (47) aliyeumia kwenye ajali ya gari miaka mingi iliyopita, na alikua amesha fanyiwa upasuaji kwenye hospitali zingine mara mbili bila mafanikio”.

Akaongeza kuwa: “Ulemavu wa goti lake ulikua umefika daraja (16) tumeweza kurekebisha hadi kafika daraja (18)”, akaongeza kuwa “Tumemfanyia upasuaji mdogo na umekua na mafanikio mazuri, anatarajiwa kuanza kutembea kwa miguu yake mwenyewe baada ya miezi miwili”.

Akasema: “Upasuaji huu unamuwezesha mgonjwa kuwa salama kwa zaidi ya miaka ishirini”, akatoa wito kwa wangonjwa “Wenye matatizo ya magoti waje wafanyiwe upasuaji, sambamba na umuhimu wa kufanya vipimo mapema”.

Tambua kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel hutoa huduma za matibabu kwa kutumia vifaa tiba vya kisasa chini ya madaktari bingwa na wauguzi mahiri kutoka ndani na nje ya nchi, jambo ambalo limeiwezesha kutoa ushindani mkubwa kwa hospitali za kimataifa.

Kumbuka kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel hualika madaktari bingwa wa maradhi tofauti, sambamba na kupokea wagonjwa wa aina mbalimbali walio katika hali tofauti za maradhi yao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: