Kituo cha tafiti za Basra na nchi za Kiarabu – kitengo cha tafiti za kisiasa na kimkakati katika chuo kikuu cha Basra kimefanya mdahalo kuhusu kitabu (mausua) ya mauaji ya Spaikar, kilicho zinduliwa hivi karibuni na kituo cha kiiraq cha kuthibitisha jinai za magaidi, chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu.
Mchokoza mada katika mdahalo huo alikua Dokta Qais Naasir na mwenyekiti wa mdahalo alikua Dokta Ali Juudah, akatoa ufafanuzi wa mausua (kitabu) hicho na umuhimu wake kwa kueleza yaliyotokea na kuhakikisha hayatokei tena.
Mchokoza mada akaeleza umuhimu wa kukumbuka jinai hiyo, ndio njia ya kudhibiti taarifa zake.
Miongoni mwa maazimio yaliyofikiwa katika mdahalo huo ni:
Watafiti na walimu wa vyuo vikuu wamehimiza umuhimu wa kufanya utafiti kuhusu mauaji ya Spaikar, hususan baada ya kupatikana nyenzo zinazosaidia kuthibitisha yaliyotokea, na hivyohivyo kwa jinai zote zilizofanywa Iraq, sambamba na kufungua idara za kuthibitisha jinai za magaidi katika vituo vya tafiti kwenye vyuo vikuu.
Kumbuka kuwa mausua (kitabu) hiki ndio mradi wa kwanza kuandika mauaji ya Spaikar, kimezinduliwa kwenye kongamano la kuadhimisha fatwa tukufu ya kujilinda awamu ya sita.