Kituo cha (Tunasoma tuwehai) chini ya kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kinatoa mitihani ya kusoma, kuandika, hesabu na utamaduni kwa wanafunzi wake katika mkoa wa Karbala.
Mkuu wa kituo Dokta Hassan Judhaili amesema: “Mradi wetu unalenga kutoa elimu kwa watu wazima, waliokuwa hawajapata nafasi ya kusoma, baada ya kufundishwa kwa muda hupewa mitihani ya kupima uwezo wao”.
Akaongeza kuwa: “Mtihani unasaidia kutambua uwelewa wa wanafunzi katika masomo waliyofundishwa na kupima maendeleo yao”.
Akabainisha kuwa: “Kituo kinazingatia changamoto za mtu mmoja mmoja katika wanafunzi wake na kuangalia namna ya kuwasaidia wale wenye changamoto za usomaji” akasema: “Kamati ya mitihani na walimu wameweka maswali ya jumla, sambamba na kuweka maswali yanayo saidia kutambua wanafunzi watakao ingia hatua ya pili”.
Tambua kuwa mradi huu unalenga kutoa elimu kwa watu wasiojua kusoma na kuandika katika mkoa wa Karbala, na kuhakikisha wanasoma hadi ngazi za juu.
kumbuka kuwa mradi wa (Tunasoma tuwehai) ni moja ya miradi muhimu kufanywa na kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa lengo la kupunguza watu wasiojua kusoma na kuandika, wanafundishwa bure kwenye vituo tofauti hapa Karbala.