Atabatu Abbasiyya tukufu imefanya hafla ya kupongeza washindi na washiriki wa shindano la (Nyota ya Maimamu a.s) lililofanywa mwezi wa Ramadhani uliopita.
Kiongozi wa idara ya harakati za vyuo chini ya idara ya mahusiano ya vyuo na shule katika kitengo cha mahusiano Muntadhiru Swafi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Shindano hilo lilihusisha wanafunzi wa vyuo vikuu, lilikua moja ya harakati iliyofanywa kwa kushirikiana na Ataba tukufu ndani ya mwezi wa Ramadhani, hafla hiyo imefanywa Jirani na malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)”.
Akaongeza kuwa: “Baada ya kupokea wageni, wakiwemo washiriki wa shindano hilo, kikafanywa kikao ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan (a.s) katika Atabatu Abbasiyya, baada ya kukaribishwa wakasikiliza mhadhara uliotolewa na kiongozi wa kituo cha Habari Jasaam Saidi, ulikua na anuani isemayo (Utambulisho wa taifa na athari ya kuupoteza), pamoja na mada iliyotolewa na Hassan Jawadi iliyokua inasema (Ufipisho wa kumtambua Mtume Mtukufu -s.a.w.w-), kisha yakatangazwa majina ya washindi, halafu wakapewa zawadi na Atabatu Abbasiyya tukufu”.
Kiongozi wa kamati ya mashindano Sajjaad Ali amesema: “Shindano hilo ni moja ya harakati ambazo hufanywa na taasisi, ilikua fursa nzuri kwa Atabatu Abbasiyya kushiriki au kutukaribisha katika malalo takatifu ya Abulfadhil Abbasi (a.s)”.
Akasema: “Shindano lilikua na vikosi (16), maswali yalikua ya kidini, kifikra na kitamaduni, zawadi ya washindi wa kwanza ilikua kwenda ziara kwa Imamu Ridhwa (a.s), na washindi wa pili na tatu walipewa zawadi kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu”.
Washiriki wa hafla hii wameishukuru Atabatu Abbasiyya tukufu na wasimamizi wa shindano hilo, kwa kutoa nafasi hii ambayo ni chachu ya kuendeleza harakati zingine.