Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Najafu imesema: Wanafunzi 2100 wanashiriki kwenye semina za Qur’ani katika mkoa wa Waasit

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani katika mkoa wa Najafu chini ya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imesema kuwa wanafunzi (2100) wameshiriki kwenye mradi wa semina za Qur’ani unaoendelea mkoani Waasit.

Msimamizi wa semina hizo katika mkoa wa Waasit Haazim Aboudi amesema: “Semina hizi ni sehemu ya harakati za Qur’ani hapa mkoani, washiriki wametoka wilaya ya Aziziyyah, Swawirah, Nu’maniyyah na mtaa wa Taju-Dini, Dabuni na Ahraar, kuna walimu zaidi ya themanini, kwa kushirikiana na muwakilishi wa Marjaa-Dini mkuu wa maeneo haya”.

Muwakilishi wa Marjaa-Dini mkuu katika wilaya ya Nu’maniyya Sayyid Muhsin Zamili amesema: “Kufanywa kwa semina hizi ni fursa kubwa ya kusoma Qur’ani, tunazifanya kwa kushirikiana na Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Najafu, tunaongeza uwezo wa usomaji wa Qur’ani”.

Akafafanua kuwa: “Tunamkakati wa kuendelea kuwasiliana na wanafunzi baada ya kumaliza semina za Qur’ani za majira ya joto, tumekubaliana kuendeleza semina za Qur’ani siku ya Ijumaa ya kila wiki, ili kulinda walicho soma katika semina hii”.

Maahadi imetuma ujumbe wa kufuatilia na kusimamia semina za Qur’ani kwenye wilaya tofauti, wanakutana na wakufunzi na kuangalia kiwango cha elimu ya washiriki, na kuwapa baadhi ya maelekezo na nasaha, aidha wanahakikisha wanatumia vizuri fursa hii waliyopewa na Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia Maahadi ya Qur’ani katika mkoa wa Najafu.

Kumbuka kuwa Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mkoa wa Najafu, mwaka huu imefanya semina za Qur’ani katika mikoa minne, wanafunzi zaidi ya elfu kumi na tatu kukoka mkoa wa Najafu, Waasit, Misaan na Diwaniyya wanashiriki.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: