Maktaba na Daru-Makhtutwaat katika Atabatu Abbasiyya tukufu imejaza shelfu vitabu vya fatwa tukufu ya kujilinda

Maoni katika picha
Maktaba na Daru-Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya chini ya kitengo cha habari na utamaduni imeonyesha shelfu maalum zilizojaa vitabu vya fatwa tukufu ya kujilinda na Hashdu-Sha’abi, ambavyo vipo mikononi mwa wasomaji.

Mtumishi wa idara ya kuazima vitabu vya maktaba bwana Nizaar Hasuun amebainisha kuwa: “Kutokana na wingi wa vitabu vinavyohusu fatwa tukufu ya kujilinda na Hashdu-Sha’abi, tumeandaa shelfu mpya za vitabu hivyo”.

Akaongeza kuwa: “Idadi za vitabu vilivyo andikwa fatwa ya Hashdu-Sha’abi vinaendelea kuongezeka, kila mwezi tunapokea idadi kubwa ya vitabu hivyo”.

Akafafanua kuwa: “Vitabu tunavyo pewa hupita katika hatua tano, kwa ajili ya kuviweka kwenye shelfu za vitabu, nazo ni:

Hatua ya kwanza: Idara ya kuazima hupokea kutoka kwa mtoaji na kutoa risiti na kumuandikia barua ya kumshukuru.

Hatua ya pili: Kitabu hupelekwa katika idara ya zawadi kwa ajili ya kupewa namba.

Hatua ya tatu: Kila kitabu hupewa namba na anuani pamoja na kuandikwa jina la muandishi, mchapishaji na tarehe ya kuchapishwa kwake.

Hatua ya nne: Vitabu hupangwa kulingana na maudhui zake, pia huwekwa kwa namba sambamba na (namba za shelfu), ili iwe rahisi kuonywa na msomaji.

Hatua ya tano: Kitabu huwekwa kwenye faharasi kwa utaratibu wa maktaba ya bunge la Marekani, kisha hupigwa bicha na kuwekwa kwenye toghuti ya maktaba kwa ajili ya kuingizwa kwenye ukumbi wa maelezo ya maktaba.

Kumbuka kuwa maktaba ya Atabatu Abbasiyya hupokea wasomi na watafiti kila siku ndani ya muda wa kazi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: