Kwa teknolojia ya uwekaji wa vyuma (Ilzarofu).. imemuokoa kijana mwenye umri wa miaka thelathini kutokana na tatizo la mfupa wa mguu

Maoni katika picha
Jopo la madaktari katika hospitali ya rufaa Alkafeel limefanikiwa kumuokoa kijana mwenye umri wa miaka zaidi ya thelathini, aliyekua na tatizo la mfupa wa mguu wake baada ya kuteseka kwa miaka sita, toka alipovunjika mfupa huo, teknolojia na vifaa tiba vilivyopo katika hospitali hii ndio sababu kubwa ya mafanikio hayo.

Daktari bingwa wa mifupa Dokta Muhammad Saad Haaris amesema: “Tulipokea mgonjwa mwenye umri wa miaka (33), aliyekua na tatizo la kuvunjika mfupa wa mguu sehemu ya chini ya goti”, akabainisha kuwa “Kijana huyo alikuwa anateseka na tatizo hilo kwa miaka sita, amefanyiwa upasuaji mara nyingi nje ya taifa bila mafanikio”.

Akaongeza kuwa: “Tumefanya upasuaji kwa kutumia vyuma (Ilzarofu), pamoja na ufuaji wa mfupa”. Akasema: “Mgonjwa ameweza kupiga hatua ya kwanza baada ya kushindwa kutembea kwa miaka sita, anatarajiwa kupona kabisa baada ya miezi sita kuanzia sasa”.

Akasisitiza kuwa: “Kutokana na teknolojia na vifaa tiba vya kisasa vilivyopo katika hospitali ya rufaa Alkafeel ndio sababu kubwa ya mafanikio haya”, akasema: “Mafanikio haya sio ya kwanza, tumesha fanyia wagonjwa wengi matibabu sawa na haya kwa mafanikio makubwa”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: