Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la Hindiyya chini ya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imefanya nadwa yenye anuani isemayo (Selebasi ya Qur’ani katika kuelekeza mazowea ya kijamii).
Mtoa mada kwenye nadwa hiyo alikua ni Dokta Basim Al-Aabidi, ameongea kuhusu mambo makuu matatu, ametaja mazowea mabaya yanayo fanana na yaliyokuwepo katika zama za ujinga.
Akaeleza namna Qur’ani tukufu ilivyo kemea mazowea hayo, na kuifanya jamii kuishi kwa amani na utulivu baada ya kuachwa.
Ametoa Ushahidi wa aya na hadithi katika mambo aliyo ongea.
Tambua kuwa Maahadi ya Qur’ani tukufu kupitia matawi yake, ni sehemu ya kituo cha Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya tukufu, inajukumu la kufundisha Qur’ani na kutengeneza jamii ya wasomi wa Qur’ani katika kila sekta.