Mkoa wa Waasit moja ya vituo vya Mimbari za nuru

Maoni katika picha
Husseiniyya Sayyid Khatibu katika wilaya ya Nu’maniyya kwenye mkoa wa Waasit, imefanya hafla ya Mimbari za nuru chini ya kituo cha miradi ya Qur’ani, kilicho katika Majmaa ya Qur’ani ya Atabatu Abbasiyya tukufu.

Mahafali za Qur’ani ni shughuli ambayo hufanywa na kituo kila wiki katika mkoa wa Balad, imepata mahudhurio makubwa ya wasomi wa Qur’ani, viongozi wa Dini na jamii.

Masikio ya wahudhuriaji yameburidishwa kwa kusikiliza sauti nyororo za usomaji wa Qur’ani tukufu, miongoni mwa waliosoma ni Karim Mansuri kutoka Jamhuri ya kiislam ya Iran na msomaji wa Atabatu Abbasiyya Ammaar Alhilliy, na msomaji Sarhani Darii muwakilishi wa umoja wa wasomaji wa Qur’ani katika mkoa wa Waasit.

Hali kadhalika kulikua na usomaji wa tenzi za kuwasifu Ahlulbait (a.s), zilizosomwa na Muhammad Baaqir Qahtwani, sambamba na tenzi zilizokua zikisomwa na msimamizi wa hafla (mc) Hasanaini Jazaairiy, zilizokua na maneno mazuri na kujaa sifa na utukufu wa usomaji wa Qur’ani na usikilizaji wake.

Kumbuka kuwa mradi wa Mimbari za nuru unahusika na kufanya mahafali za usomaji wa Qur’ani ndani na nje ya mkoa wa Karbala, katika Ataba, Mazaru, Husseiniyya na misikiti, kwa kushirikiana na taasisi za Qur’ani hapa mkoani na kwenye vitengoji vyake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: