Wawakilishi wa mawakibu Husseiniyya wanatembelea kitengo cha kutengeneza madirisha ya makaburi na milango yake

Maoni katika picha
Ugeni wa wawakilishi wa Mawakibu na vikundi vya Husseiniyya katika mji wa Karbala na viongozi kutoka mikoa tofauti, wametembelea kitengo cha kutengeneza madirisha ya makaburi na milango katika Atabatu Abbasiyya tukufu.

Rais wa kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya Sayyid Aqiil Abdulhussein Yaasiriy ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Ziara hii ni kwa ajili ya kuangalia mafanikio ya kitengo hiki, ziara imefanywa na ujumbe wa watu wa aina mbili, kwanza wawakilishi wa Mawakibu za Karbala na vikundi vyake, pili wawakilishi wa idara za mikoani zilizo chini ya kitengo chetu”.

Akaongeza kuwa: “Wageni hao wametembelea kiwanda kilicho tengeneza madirisha mengi, na kuangalia utendaji wake na kusikiliza maelezo ya hatua za utengenezaji kuanzia hatua ya kwanza hadi mwisho”.

Akabainisha kuwa: “Ugeni umepongeza kazi zinazofanywa na kitengo hiki, wamesema kuwa hakika kitengo hiki kinafaa kujivunia sambamba na uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: