Kwa kuhudhuria katibu wake mkuu: Atabatu Abbasiyya tukufu imehitimisha wiki ya kwanza ya program yake

Maoni katika picha
Ukumbi wa Imamu Hassan (a.s) katika Atabatu Abbasiyya tukufu, umehudhuriwa na katibu mkuu Sayyid Mustwafa Murtadha Dhiyaau-Dini na baadhi ya wajumbe wa kamati kuu, katika kuhitimisha wiki ya kwanza ya program maalum ya watumishi wake.

Katika kikao hicho zimetolewa nasaha na maelekezo muhimu kutoka kwa katibu mkuu na wajumbe wa kamati kuu akiwemo msimamizi wa program hiyo Sayyid Liith Mussawi.

Mwishoni mwa kikao hicho zikatolewa zawadi kwa washindi wa mashindano yaliyofanywa wakati wa program.

Washiriki wamepongeza na kushukuru program hiyo, wamesema kuwa inasaidia kupunguza mzigo wa kazi na kujenga ushirikiano baina yao, wameomba program hii iendelee kwani inafaa sana kwa watumishi.

Tambua kuwa program hiyo imedumu kwa muda wa siku tano, ilikua na vipengele vingi, kulikuwa na mihadhara ya kiitikadi, kutembelea malalo ya Imamu Ali bun Abu Twalib (a.s) na Maraaji-Dini watukufu katika mji wa Najafu, hauza pamoja na kufanya kikao cha usomaji wa Qur’ani, mashindano ya kidini na kutembelea miradi ya Atabatu Abbasiyya tukufu, program itaendelea wiki zijazo na inatarajiwa kuhusisha idadi kubwa zaidi ya watumishi.

Kumbuka kuwa kikao cha kuhitimisha program hiyo kimehudhuriwa pia na makamo katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Mhandisi Abbasi Muusa na wajumbe wa kamati inayosimamia program hiyo, nao ni Dokta Muhammad Hassan Jaabir rais wa kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu, Dokta Mushtaq Ali rais wa Majmaa ya Qur’ani, Sayyid Aqiil Abdulhussein Alyaasiriy rais wa kitengo cha Habari na utamaduni, Sayyid Muhammad Jaluhani makamo rais wa kitengo cha mahusiano.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: