Yanaabia-Rahma imeanza ratiba yake awamu ya pili

Maoni katika picha
Idara ya Qur’ani chini ya ofisi ya maelekezo ya Dini tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imeanza hatua ya pili ya semina ya (Yanaabia-Rahmah) kwa wasichana wenye umri wa miaka (10 -11 – 12), kwa ushiriki wa wanafunzi wa kike katika mkoa wa Karbala na itadumu kwa muda wa siku kumi na tano.

Kiongozi wa idara hiyo bibi Fatuma Mussawi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Hatua hii ni muendelezo wa hatua zilizotangulia, zilizo kua na muitikio mkubwa kutoka kwa washiriki na wazazi wao, jambo ambalo linasaidia kutumia vizuri kipindi cha likizo ya majira ya joto, kwa kufanya mambo yenye manufaa zaidi kwa washiriki, ratiba ya masomo inaendana na umri wao na inatekelezwa na walimu waliobobea kwenye sekta hiyo”.

Akabainisha kuwa: “Maandalizi ya awamu hii yalianza muda mrefu, tulifungua mlango wa usajili, baada ya kukamilisha usajili ndio tumeanza kutekeleza ratiba, kuna vipengele vya Dini, Utamaduni, Maelekezo na Ibada pamoja na kipengele cha michezo na mashindano”.

Akaongeza kuwa: “Siku ya kwanza baada ya kuwakaribisha washiriki na kufanya shughuli za ufunguzi, tulifanya ziara kwenye malalo ya Abulfadhil Abbasi kwa pamoja, na tukatembelea maeneo ya Atabatu Abbasiyya pamoja na Maktaba ya Ataba, halafu tukasoma surat Yaasin kwa pamoja”.

Kumbuka kuwa hii ni moja ya semina nyingi zinazofanywa na idara, maandalizi yote muhimu yamekamilika, kuanzia selebasi, walimu, sambamba na mambo mengine ya kiutawala, usafiri wa kwenda na kurudi sanjari na kuandaa zawadi na vyeti vya ushiriki.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: