Atabatu Radhawiyya takatifu yampongeza rais wa kitengo cha Dirasaat-Qur’aniyya katika chuo kikuu cha Ummul-Banina

Maoni katika picha
Atabatu Radhawiyya takatifu imempongeza rais wa kitengo cha Dirasaat-Qur’aniyya katika chuo kikuu cha Ummul-Banina (a.s) cha wasichana kwa njia ya mtandao katika mji wa Najafu, ambacho kipo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu Ustadh Ali Hamiid Albayati, kwa kupata tuzo ya Ridhwani ya kimataifa.

Amepongezwa wakati akikabidhiwa zawadi ya ushindi na cheti, mbele ya makamo kiongozi mkuu wa mambo ya kimataifa katika majmaa ya tafiti za kielimu iliyochini ya Atabatu Radhawiyya Sayyid Muhammad Dhulfiqaar.

Ustadh Ali Albayati ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Pongezi hizi zinatokana na ushindi aliopata kwenye shindano la kimataifa, lililokua na ushiriki mkubwa kutoka kwa watu wa madhehebu tofauti za kiislamu, jumla ya maustadhi (2412) walishiriki kwenye sekta ya kufundisha Qur’ani tukufu na tafsiri yake”.

Akaongeza kuwa: “Tumeongeza kitu kwenye zawadi hii na kuipa jina la (Mwalimu wa Qur’ani anatakiwa kuthaminiwa), hii ni sehemu ya kwanza ya zawadi, baada ya kuchaguliwa washindi (28) kutoka nchi tofauti duniani”.

Kumbuka kuwa zawadi ya Ridhwani ni zawadi ya kimataifa ambayo hutolewa na Atabatu Radhawiyya kila baada ya miaka miwili, kwa walimu wa Qur’ani wanaokidhi vigezo na wanaochukuliwa kwa mfano mwema na (kigezo kwa walimu wa Qur’ani).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: