Huzuni za kifo cha Aljawaad.. Atabatu Abbasiyya tukufu imewekwa mapambo meusi

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu na malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) imevaa vazi la msiba katika kukumbuka kifo cha Imamu Aljawaad (a.s) aliyekufa mwishomi mwa mwezi huu.

Muonekano wa huzuni umeenea ndani ya haram tukufu na kwenye malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa zaidi ya siku tatu, kutokana na msiba huo mkubwa kwa Maimamu wa nyumba ya Mtume (a.s) na wafuasi wao, hakika ni msiba wa kufiwa na Imamu wa tisa mtakasifu, ambaye ni miongoni mwa Maimamu waliobashiriwa na Mtume (s.a.w.w) watakaokuja baada yake.

Watumishi wa kitengo cha kusimamia haram tukufu wameweka mapambo yanayo ashiria huzuni na majonzi, kwenye maeneo yote ya ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), Atabatu Abbasiyya tukufu inatoa pole kwa Mtume na watu wa nyumbani kwake (a.s) kutokana na msiba huu.

Kama kawaida ya Atabatu Abbasiyya tukufu katika matukio ya kumbukizi za vifo vya watu wa nyumba ya Mtume (a.s), huandaa ratiba ya uombolezaji na utoaji wa huduma.

Kumbuka kuwa Imamu Muhammad Aljawaad bun Ali Ridhwa (a.s) ni Imamu wa tisa miongoni mwa Maimamu wa nyumba ya Mtume (a.s), alizaliwa mwaka wa (195h) akafa kishahidi mwishoni mwa mwezi wa Dhulqaada mwaka (220h), baada ya kupewa sumu na mke wake (Ummul-Fadhil) kwa amri ya Mu’taswimu Abbasi, hivyo akaaga dunia akiwa na umri wa miaka (25), muda wa Uimamu wake ulikua miaka (17).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: