Idara ya teknolojia na taaluma za mitandao chini ya kitengo cha Habari katika Atabatu Abbasiyya, inatoa wito kwa kila anayependa kufanyiwa ziara kwa niaba, mbele ya malalo ya Imamu Muhammad Aljawaad (a.s) katika kumbukumbu ya kifo chake kwenye mji wa Kadhimiyya.
Tambua kuwa usajili unafanyika kupitia link ya ziara kwa niaba, ambayo ni sehemu ya mtandao wa kimataifa Alkafeel, link hiyo ni: https://alkafeel.net/zyara/
Kila atakaejisajili atafanyiwa ziara na mmoja wa watumishi wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) miongoni mwa Masayyid waliokwenda huko kwa ajili hiyo.
Watatoa pole na kufanya ziara ya Imamu Jawaad na babu yake Imamu Mussa bun Jafari (a.s), na swala ya rakaa mbili kwa niya ya kukidhi haja na kurahisisha mambo, kwa niaba ya kila aliyejisajili na wapenzi wa Ahlulbait (a.s) na wafuasi wao.