Huzuni za Karbala zimetanda ndani ya haram ya Kaadhimiy takatifu kwa kifo cha Imamu Aljawaad (a.s)

Maoni katika picha
Watu wa Karbala kupitia maukibu yao ya pamoja, jioni ya leo Jumanne, wameomboleza kumbukumbu ya kifo cha Imamu Aljawaad (a.s), mbele ya malalo yake takatifu katika mji wa Kadhimiyya, kwa kushirikiana na kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya chini ya Ataba mbili takatifu.

Maukibu ya kuomboleza imehusisha vikundi tofauti kutoka Karbala, Pamoja na watu wa mkoa huo wakiongozwa na Sayyid Aqiil Yasiriy, wametoa rambirambi na kuonyesha huzuni kutokana na msiba huo mkubwa unaoumiza roho za wafuasi wa Ahlulbait (a.s), uliotokea mwisho wa mwezi wa Dhulqaadah mwaka wa (220h).

Waombolezaji baada ya kumaliza matembezi yao wamefanya majlisi ndani ya uwanja wa haram ya Maimamu wawili Alkadhimaini (a.s) mbele ya mlango wa Muraad, imepambwa kwa qaswida na tenzi za kuomboleza, zilizo amsha hisia za huzuni kwa waombolezaji wote.

Kumbuka kuwa Maukibu ya kuomboleza ni utamaduni uliozoeleka kwa watu wa Karbala katika kuomboleza kumbukumbu za Ahlulbait (a.s), Maukibu hii inafadhiliwa na Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, kwa kuipa mahitaji ya lazima ili iweze kufanya shughuli za kuomboleza, hususan zinazofanywa nje ya Mkoa wa Karbala, likiwemo tukio hili la kumbukumbu ya kifo cha Imamu Aljawaad (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: