Kifo cha Mlango wa elimu Imamu Aljawaad (a.s) kilitokea mwishoni mwa mwezi wa Dhulqadah

Maoni katika picha
Wapenzi na wafuasi wa Maimamu wa Ahlulbait (a.s), mwishoni mwa mwezi wa Dhulqadah kila mwaka huomboleza kifo cha Imamu wa tisa miongoni mwa Maimamu waongofu Muhammad Aljawaad (a.s).

Kifo chake ni huzuni kubwa inayoumiza sana umma wa kiislamu, hakika kifo chake kilikua sawa na kufunikwa ukurasa miongoni mwa kurasa za ujumbe wa Uislam, alifariki mwaka (220) hijiriyya katika mji wa Bagdad mwanzoni mwa utawala wa Mu’taswimu Abbasi (laana iwe juu yake).

Riwaya zinaonyesha kuwa Mu’taswimu Abbasi alijaribu mara nyingi kumuua Imamu Aljawaad (a.s), kisha akaamua kutumia mbinu ya kumpa sumu kwa kumtumia Ummulfadhil.

Jafari bun Ma-Amuun akawasiliana na dada yake (Ummulfadhil) mke wa Imamu Aljawaad (a.s), Jafari alikua anajua wivu wake kwa mke mwingine wa Imamu (Mama wa Imamu Alhaadi), akamlaghai na kumpa mbinu za kutekeleza lengo lao, naye akakubali.

Jafari akampa sumu kali kwa amri ya Mu’taswimu, kisha Imamu (a.s) akawekewa kwenye chakula, inasemekana aliwekewa kwenye zabibu zilizokua zikipendwa na Imamu, alipo kula alihisi maumivu makali na akaanza kutapika damu, akalala na akawa anajigeuza kulia na kushoto hadi akaaga dunia, ulikua mwaka wa (220) hijiriyya.

Imepokewa kuwa mwanae Imamu Ali Alhaadi (a.s), alimuandaa kwa kumuosha na kumvisha sanda kama alivyo husiwa, kisha akamswalia pamoja na wafuasi wake.

Jeneza lake lilishindikizwa na umati mkubwa wa watu, maelfu ya watu walijitokeza na kwenda kumzika kwenye makaburi ya Makuraishi, sehemu alipozikwa babu yake Imamu Mussa bun Jafari (a.s), akazikwa pembeni ya babu yake sehemu ambayo inajengo kubwa lenye minara ya dhahabu kwa sasa, maelfu wa waislamu huenda kumzuru kila siku na kuomba haja zao, hurudi wakiwa na furaha kwa matumaini ya kutatuliwa haja zao”.

Hivyo ndivyo ukurasa mweupe ulivyofungwa na nyota ya Ahlulbait (a.s) ilivyozimika, amani iwe juu yake siku aliyozaliwa na siku aliyouawa na siku atakayo fufuliwa kutoa shuhuda kwa umma.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: