Atabatu Abbasiyya inafanya majlisi za kuomboleza kifo cha Imamu Aljawaad (a.s)

Maoni katika picha
Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu umefanya majlisi ndani ya ukumbi wa utawala, kuomboleza kifo cha Imamu wa tisa Muhammad Aljawaad (a.s), iliyo hudhuriwa na watumishi wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na mazuwaru wake.

Majlisi imefanywa kwa siku mbili mfululizo, na kuhitimishwa asubuhi ya leo siku ya Alkhamisi, ilikua inafunguliwa kwa Qur’ani tukufu, halafu unafuata mhadhara wa Sayyid Adnani Mussawi kutoka kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu, ameongea kuhusu Maisha ya Imamu Aljawaad (a.s) katika zama za utawala wa Bani Abbasi, historia yake imejaa nuru na kheri, akasisitiza umuhimu wa kufuata mwenendo wake (a.s).

Majlisi ilikua inahitimishwa kwa tenzi za kuomboleza zilizo amsha hisi za huzuni ya msiba huo mkubwa katika ulimwengu wa kiislamu, hakika ulitikisa dunia, watu wakatoka kila sehemu kwenda kushindikiza muili mtakatifu wa Imamu (a.s), Imamu alifariki kishahidi mwaka (220h), hakika alikua kimbilio la waislamu wote.

Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya tukufu ni kawaida yake katika kumbukumbu za vifo vya watu wa nyumba ya Mtume (a.s), kuandaa ratiba maalum ya uombolezaji ndani na nje ya mji mtukufu wa Karbala.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: