Kutia sahihi makabidhiano ya dirisha la malalo ya bibi Zainabu (a.s)

Maoni katika picha
Atabatu Zainabiyya takatifu kupitia kiongozi wake Sayyid Muhsin Harbu, ametia sahihi ya kupokea dirisha la malalo takatifu ya bibi Zainabu (a.s), baada ya kumaliza kutengenezwa na watumishi wa kitengo cha utengenezaji wa madirisha ya kwenye makaburi na milango mitukufu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, ametia sahihi mbele ya katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Mustwafa Murtadhwa Dhiyaau-Dini na baadhi ya wajumbe wa kamati kuu pamoja na mkuu wa ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria.

Sayyid Harbu ameuambia mtandao wa Alakafeel kuwa: “Kwa msaada wa Mwenyezi Mungu leo tumeweka sahihi ya kupokea dirisha la malalo ya Aqilah Zainabu (a.s) ndani ya malalo ya msimamizi wake Abulfadhil Abbasi (a.s), tumekabidhiwa dirisha kamili, hakika hili ni jambo kubwa sana ambalo tumepokea kutoka kwa Abulfadhil Abbasi (a.s) kwenda kwa dada yake bibi Zainabu (a.s)”.

Akaongeza kuwa: “Tunamshukuru kila aliyechangia mafanikio haya mazuri, kazi yote imefanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu na watumishi wake, hakika wamekua msitari wa mbele katika kusaidia malalo zote za Maimamu wa Ahlulbait (a.s)”.

Upande wa Atabatu Abbasiyya tukufu sahihi imewekwa na mkuu wa kitengo cha kutengeneza madirisha ya makaburi na milango mitukufu bwana Huquqi Kadhim, na upande wa Ataba ya bibi Zainabu (a.s), mtia sahihi alikua ni Sayyid Muhsin Harbu.

Kumbuka kuwa ugeni wa Atabatu Zainabiyya ulikua umesha kagua dirisha hilo kila sehemu kabla ya tukio hilo la kutiliana saini.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: