Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Najafu imefanya zaidi ya majlisi mia moja za uombolezaji

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tukufu katika Mji wa Najafu chini ya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imefanya zaidi ya majlisi mia moja za kuomboleza kifo cha Imamu Muhammad Aljawadi (a.s).

Kiongozi wa idara ya harakati Sayyid Zaidi Maduhi Rimahi amesema kuwa: “Majlisi hizo ni sehemu ya mradi wa semina za Qur’ani katika majira ya joto, zinazo fanywa na Maahadi kwenye mikoa tofauti, hivyo ilipangwa ratiba maalum kwa ajili ya maombolezo hayo”.

Akaongeza kuwa: “Vikao vya uombolezaji vimefanywa sambamba na vikao vya usomaji wa Qur’ani katika mkoa wa Najafu, Waasit, Diwaniyya, Misaan na kuhudhuriwa na Zaidi ya wanafunzi elfu kumi na tatu”.

Akabainisha kuwa: “Wahadhiri wameongea mambo mbalimbali kuhusu Maisha ya Imamu Aljawaad (a.s) sambamba na kuhimiza kuyapenda maadhimisho ya Husseiniyya, yanayotokana na kauli ya Mtume (s.a.w.w) isemayo: (Mimi nakuachieni vizito viwili, kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi changu).

Kumbuka kuwa Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Najafu imefanya semina za Qur’ani kwenye mikoa minne, zaidi ya wanafunzi elfu kumi na tatu wamejiunga kwenye semina hizo kutoka mkoa wa Najafu, Waasitu, Misaan na Diwaniyya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: