Kuendelea kwa program ya watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu

Maoni katika picha
Program ya watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu inaendelea kwa wiki ya pili, nayo ni program kubwa kuwahi kufanywa kwa watumishi hao, wanapigwa msasa wa masomo ya Aqida, Malezi na Akhlaqi.

Ratiba ya wiki ya pili ni muendelezo wa wiki ya kwanza, iliyokua na warsha, mihadhara, nadwa, mashindano na ratiba za mapumziko na kutembelea malalo ya Imamu Ali (a.s) na ofisi mbalimbali za Maraajii-Dini watukufu katika mji wa Najafu.

Washiriki walipongeza sana program hiyo, walisema inapunguza ugumu wa kazi zao na kujenga mapenzi na ushirikiano baina yao, wakaomba iendelee kutokana na umuhimu wake kwa watumishi.

Kumbuka kuwa program hii inafanyika siku tano katika wiki kwa kila kikundi, inalenga kupiga msasa wa mambo ya kidini kwa washiriki sambamba na mambo ya kielimu na kimaadili, na kuongeza itiifu katika kufanya kazi chini ya bendera ya Abulfadhil Abbasi (a.s) sambamba na kuboresha huduma kwa mazuwaru.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: