Atabatu Abbasiyya tukufu inafanya semina ya (Tunaanza kutokea hapa) ya wasichana kwa ushiriki wa wanafunzi 200

Maoni katika picha
Idara ya shule za Alkafeel za Dini chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, inafanya semina ya Dini, iliyopewa jina la (Tunaanza kutokea hapa) kwa wanafunzi wa kike 200 kutoka mkoa wa Karbala.

Kiongozi wa Idara hiyo, bibi Bushra Kinani ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Semina imetokana na maelekezo ya uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, unaohimiza kutumia vizuri kipinzi cha likizo za majira ya joto kwa kundi hili la wasichana, na kuchangia katika kuongeza maarifa mbalimbali”.

Akaongeza kuwa: “Umri lengwa ni wasichana wenye miaka (12 hadi 25), semina itadumu kwa muda wa mwezi mzima, watafundishwa masomo ya (Fiqhi, Aqida, Sira, Akhlaq, maarifa ya Qur’ani, Imamu Mahadi (a.f) na kazi za mikono), aidha kutakua na vipindi vya michezo, mashindano na midahalo”.

Akabainisha kuwa: “Semina inafanywa katika shule ya Alqamar iliyochini ya Al-Ameed katika kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, wameandaliwa baadhi ya mahitaji ya lazima katika usomaji”.

Akafafanua kuwa: “Kitengo cha usafiri katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimechukua jukumu la kuwabeba kutoka majumbani kwao hadi sehemu ya semina na kuwarudisha, semina hii imepata muitikio mkubwa, jambo ambalo linatia moyo kwa wasimamizi wa semina, wa kufanya kila wawezalo kwa ajili ya kufikia malengo yaliyokusudiwa”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: