Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu amepokea bendera ya Ghadiir Al-Agharu

Maoni katika picha
Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Mustwafa Murtadhwa Dhiyaau-Dini leo siku ya Jumamosi baada ya Adhuhuri, amepokea bendera ya Ghadiir Al-Agharu ndani ya ukumbi wa utawala, iliyoandikwa (Niliyekua kuongozi wake basi Ali ni kiongozi wake), imekabidhiwa na wajumbe kutoka Atabatu Alawiyya wakiongozwa na Dokta Salim Jaswani.

Wajumbe hao wametoa mualiko kwa katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu wa kushiriki kwenye mkutano wa watumishi wa Ataba tukufu, utakaojadili uboreshaji wa huduma kwa mazuwaru na kujenga ushirikiana baina ya Ataba tukufu, mkutano huo utafanywa tarehe (12) ya mwezi wa Dhulhijja katika Atabatu Alawiyya tukufu.

Kumbuka kuwa Atabatu Alawiyya hutoa bemdera ya Iddul-Ghadiir kwa Ataba tofauti, mikoa tofauti na miji tofauti ya Iraq, ikiwa ni sehemu ya kusherehekea tukio tukufu la mwezi kumi na nane Dhulhijja.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: