Mtandao wa kimataifa Alkafeel (1 Dhulhijja 1443h/ 1 Julai 2022m).
Baada ya Atabatu Zainabiyya kutia saini kupitia kiongozi wake Sayyid Muhsin Harbu, ya kupokea dirisha la malalo yake takatifu, kufuatia kukamilika uundwaji wake uliofanywa na kitengo cha kutengeneza madirisha ya makaburi matukufu na milango yake katika Atabatu Abbasiyya tukufu, mjumbe wa kamati kuu ya Atabatu Abbasiyya bwana Huquqi Kaadhim ambaye ni msimamizi wa kitengo tajwa, amefanya mahojiano maalum na mtandao wa kimataifa Alkafeel, amesema: “Kwa mara ya kwanza katika historia ya Iraq dirisha kama hili linatengenezwa, haya ni mafanikio makubwa kuwa na dirisha kama hili lililoandikwa (limetengenezwa Iraq)”.
Akasema: Kuna mambo mawili, kwanza jambo la kiroho, pili la kimazingira katika uwajibikaji wa Atabatu Abbasiyya tukufu kwenye kutengeneza dirisha la malalo ya bibi Zainabu (a.s).
Jambo la kiroho, Abbasi (a.s) alikua ndio msimamizi wake katika Maisha yake.
Na jambo la kimazingira, hakika Atabatu Abbasiyya inakiwanda maalum cha kutengeneza madirisha ya makaburi matukufu, mafanikio yote haya yanatokana na hekima na maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria ambaye daima amekua akiusia kuhuisha neno la (imetengenezwa Iraq), jambo zuri kwa sasa taifa la Iraq kwa mara ya kwanza linafanikiwa kupeleka dirisha nje ya taifa lililo tengenezwa hapa Iraq, na dirisha hilo limeandikwa (limetengenezwa Iraq), dirisha hili liko sawa na madirisha mengine na limetengenezwa kwa mbao, dhahabu, fedha na vitu vingine, aidha limetengenezwa kisasa kabisha ukilinganisha na madirisha mengine, limetiwa nakshi nzuri zilizo sanifiwa na Dokta Amiin Nuriy mwalimu wa mapambo na usanifu katika chuo kikuu cha Bagdad, na maandishi yamewekwa na rais wa taasisi ya waandishi Dokta Raudhani Bahiyya, na mapambo ya ndani yamewekwa na Ustadh Hussam Raudhan, kazi zote zimefanywa na mafundi wa Kiiraq, tena mafundi wote ni watumishi wa kitengo cha utengenezaji wa madirisha ya makaburi chini ya uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu.
Kazi hii ilitakiwa kukamilika ndani ya miezi (30), lakini imekamilika ndani ya miezi (21), chini ya muda uliokadiriwa, kutokana na juhudi za watumishi wetu watukufu na uaminifu wao, ikumbukwe kuwa kazi yeyote haikosi changamoto, kulikua na changamoto ya uagizaji wa vifaa kutoka nje ya Iraq, kwa mfano mbao na vinginevyo, kwa msaada wa uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu tuliweza kushinda changamoto zote, hakika tumepata msaada mkubwa kutoka Ataba, vifaa tulivyotumia katika utengenezaji wa dirisha hili ni:
Mbao halisi za aina tofauti.
Madini ya silva karibu kilo 3000.
Madini ya kopa karibu kilo 3000.
Madini ya fedha karibu kilo 500.
Madini ya dhahabu karibu kilo 5.
Mina za kioo zenye taraja 1100.
Marumaru za (Oksi) zimewekwa pembezoni na chini kwa ndani.
Baada ya kufikiwa mafanikio haya, furaha tuliyonayo haielezeki, hii ni kazi tukufu kana kwamba ndoto imekua kweli, kuna maneno yanipasa kuyasema:
(kwanza) shukrani za pekee zimuendee Mwenyezi Mungu mtukufu aliyetuwezesha kufanya huduma hii tukufu.
(pili) zimuendee bwana wa maji na uaminifu, aliyetukubalia kumtumikia na jina letu la kazi likafungamana na jina lake tukufu.
(tatu) zimuendee Mheshimiwa kiongozi mkuu wa kisheria, kwa uongozi wake mtukufu na hekima zake takatifu katika Atabatu Abbasiyya, msaada usiosimama anaotoa kwa miradi ya Ataba.
(nne) ziuendee uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kusaidia watumishi wa kitengo chetu katika nyanja zote, pamoja na vitengo vyote vilivyo toa ushirikiano wa hali na mali kwa kitengo cha kutengeneza madirisha ya makaburi.
(tano) ziendee uongozi wa Maqaam ya bibi Zainabu (a.s) na wafadhili waliojitolea pesa kwa uaminifu wao kwetu, tunamshukuru Mwenyezi Mungu tumefanya kazi kwa uaminifu mkubwa.
(sita) zimuendee kila aliyefanya kazi ya utengenezaji wa dirisha hili hususan Dokta aliyefanya usanifu Amiin Nuriy, Dokta wa hati Raudhan Bahiyya, Ustadh wa mapambo Hussam Raudhan Bahiyya, Ustadh Ali Swafaar, Mhandisi Ali Salum, viongozi wote na watumishi wa kitengo cha utengenezaji wa madirisha ya makaburi matukufu kwa kazi nzuri waliyofanya.
Mwisho nasema:
Bibi yangu mtakatifu
Ewe muaminifu na mtukufu wa wanawake baada ya mama yako mtakatifu Zaharaa
Ewe jabali wa Subira na Imani
Hakika sisi tunakuja kwako tukiwa na bidhaa hii, tukubalie na utupe sadaka kwa shifaa yako, mama yako Zaharaa, baba yako Karaar, babu yako Mukhtaar na kaka zako (a.s).