Kuendelea kwa shindano la Imamu Hassan Almujtaba (a.s) kwa siku ya pili mfululizo

Maoni katika picha
Kuendelea kwa shindano la Imamu Hassan Almujtaba (a.s) la usomaji wa Qur’ani, linalo ratibiwa na Maahadi ya Qur’ani tawi la Baabil, chini ya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya tukufu.

Mjumbe wa kamati ya maandalizi ya shindano na kiongozi wa ofisi ya usomaji katika Maahadi ya Qur’ani tawi la Baabil Sayyid Luayi Abduhamza Hasuun amesema: “Kamati ya maandalizi imekamilisha kila kitu kinacho hitajika kwenye shindano hilo sambamba na kuunda kamati ya majaji watano, yupo anayehusima na kanuni za tajwidi, kusimama na kuanza, sauti na naghma, ubora ya uhifadhi”.

Akaongeza kuwa: “Taasisi za Qur’ani zilizopata mualiko wa kushiriki kwenye mashindano zimeleta karibu wasomaji (64) wanaosoma kwa mahadhi ya Iraq na Misri, na huo ndio upekee wa shindano hilo kwa ushuhuda wa kila mtu”.

Naye muwakilishi wa muungano wa wasoma Qur’ani katika mji wa Diwaniyya bwana Yasiri Muhanna amesema: “Hili ni shindano la pekee hapa nchini kwani linahusisha mahadhi ya Iraq na Misri”.

Akafafanua kuwa: “Shindano hili limeibua vipaji vya usomaji wa Qur’ani, akatoa wito kwa taasisi zote za Qur’ani zifuate nyayo za Maahadi ya Qur’ani chini ya Majmaa ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya kwa kufanya mashindano kama haya”.

Kumbuka kuwa shindano lilianza jana siku ya Jumamosi katika mkoa wa Baabil, kwa ushiriki wa mikoa (15) ya Iraq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: