Semina ya utoaji wa huduma ya kwanza na uokozi kwa watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu

Maoni katika picha
Wataalam wa uokozi na mafunzo ya utabibu, chini ya kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, wanatoa semina ya utoaji wahuduma ya kwanza na uokozi.

Mkufunzi wa semina na kiongozi wa idara hiyo Kabatan Muhammad Aamir amesema: “Lengo la semina hii ni kutoa elimu ya uokozi kwa watumishi wote wa Atabatu Abbasiyya tukufu, na kuwafanya waweze kutoa huduma zora za uokozi wakati wakutekeleza majukumu yao, na katika maisha ya kila siku”.

Akaongeza kuwa: “Semina inamada nyingi, miongoni mwake ni: upitishaji wa hewa, upumuaji, mzunguko wa damu, majeraha ya kichwani, macho na kuvunjika viungo”.

Akaendelea kusema: “Wanapewa masomo ya nadharia kwa asilimia %30 na vitendo asilimia %70 kulingana na utaritibu wa kimataifa”, akasema: “Semina hiyo imeendeshwa kwenye majengo ya Shekhe Kuleini”.

Akaashiria kuwa: “Tumetoa vyeti vya pongezi mwishoni mwa semina kwa waliofaulu kwa zaidi ya asilimia %70, na vyeti vya ushiriki kwa waliopata chini ya asilimia hizo, tambua kuwa kazi hii unadili na roho za watu”.

Kumbuka kuwa kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kinaendelea kuratibu semina na warsha mbalimbali kwa watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu, katika sekta tofauti.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: