Zawadi kutoka malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa wanandoa wapya sambamba na kuadhimisha ndoa ya nuru mbili

Maoni katika picha
Kitengo cha mahusiano katika Atabatu Abbasiyya kwa kushirikiana na ofisi ya mahusiano ya vyuo na shule, kimetoa zawadi za tabaruku kutoka kwenye malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa wanandoa watarajiwa kutoka mkoa wa Bagdad sambamba na maadhimisho ya kumbukumbu ya ndoa ya nuru mbili Imamu Ali na Fatuma (a.s).

Kiongozi wa idara ya mawasiliano ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Hili ni moja ya matukio mengi ambayo hufanywa na kitengo cha mahusiano kwenye maadhimisho mbalimbali, kitengo kimetuma ujumbe katika mahakama ya Kadhimiyya katika mji mkuu wa Bagdad, kwenda kutoa zawadi kwa wanandoa wapya waliofunga ndoa zao ndani ya malalo takatifu ya Abulfadhil Abbasi (a.s) sambamba na kuwatakia Maisha mema katika ndoa zao”.

Akaongeza kuwa: “Wanandoa kadhaa wamepewa zawadi hizo sambamba na kuwakumbusha ilivyokua ndoa ya Imamu Ali na Zaharaa (a.s), ndoa iliyo onganisha nuru ya Utume na Uimamu, inafaa kuwa kigezo chema cha kujenga mahusiano mazuri kwa wanandoa”.

Qadhi Saadi Muhyi Aljaburi wa Mahakama ya Kadhimiyya amesema kuwa “Tumefurahi sana kupokea ugeni huu kutoka kwenye malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), ukiwa na zawadi maridhawa kwa wanandoa wapya, hakika zawadi hizo zina athari kubwa kwa wanandoa hao”.

Wanandoa wapya na wazazi wao wameshukuru Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kuwajali na kuwaletea zawadi hizo, wamesema kuwa tukio hilo limewafurahisha sana.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: