Kukamilisha ufungaji wa shehena ya dirisha la malalo ya bibi Zainabu (a.s)

Maoni katika picha
Watumishi wa kitengo cha kutengeneza madirisha ya makaburi na milango mitukufu chini ya Atabatu Abbasiyya wamekamilisha ufungaji wa shehena ya dirisha la malalo ya bibi Zainabu (a.s), baada ya kulifungua kipande kimoja kimoja mbele ya kiongozi wa idara ya Atabatu Zainabiyya Sayyid Muhsin Harbu na msimamizi wa kitengo hicho Huquqi Kaadhim. Rais wa kitengo Sayyid Naadhim Ghurabi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu mtukufu na baraka za Abulfadhil Abbasi (a.s), na msaada wa moja kwa moja kutoka kwa kiongozi mkuu wa kisheria Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi na katibu wake mkuu Sayyid Mustwafa Murtadha Dhiyaau-Dini, tumekamilisha kazi yote ya utengenezaji wa dirisha sehemu za madini na mbao kama ilivyopangwa na chini ya muda uliokadiriwa”.

Akaendelea kusema: “Leo tupo katika hatua ya kufungasha dirisha kwenye masanduku maalum kwa ajili ya kulipeleka kwenye malalo ya bibi Zainabu (a.s), kikosi cha Abbasi kitachukua jukumu la kulisafirisha”. Akaongeza kuwa: “Kazi ya kufungasha shehena imeanza baada ya kufungua dirisha na kutenganisha sehemu zake zote kisha zikasafishwa kwa kutumia vifaa maalum kulingana na kila kipande na aina ya madini yake, halafu kinafungwa kwa plastiki na kuwekwa kwenye sanduku, kisha kila sanduku linawekwa namba na kufungwa vizuri”.

Akamaliza kwa kusema: “Tumeunda kamati ya mafundi itakayo safiri na masanduku hayo na kusimamia utunzwaji wake, na kamati nyingine itakayo simamia ufunguaji wa dirisha la zamani lililopo kwenye malalo ya bibi Zainabu (a.s) na kufunga dirisha jipya”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: