Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Najafu chini ya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imefanya hafla ya kuhitimu mamia ya wanafunzi wa Dini kupitia mradi wa Qur’ani.
Mkuu wa Maahadi Sayyid Muhandi Almayali amesema: “Mradi huu unalenga kuwajenga wanafunzi kielimu katika sekta ya usomaji na maarifa ya Qur’ani, sambamba na kushajihisha waandishi wa hauza kuandika vitabu vya maarifa ya Qur’ani tukufu, kwa kuweka shindano la kitabu bora cha maarifa ya Qur’ani na kuongeza idadi ya vitabu vya maarifa ya Qur’ani kwenye maktaba za kiislamu.
Akaongeza kuwa: “Mradi huo kwa mwaka huu ulipewa jina la (Yubalighuna), ulikua maalum kwa wasomi wa Qur’ani, wamepewa semina maalum za Qur’ani na kuwatuma kwenye mikoa minne hapa nchini, ambayo ni: Basra, Dhiqaar, Waasit na Misaan, katika nusu ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadhani”.
Tambua kuwa hafla hii inafanywa kwa mara ya sita mfululizo, sanjari na kuhitimu awamu ya sita ya mradi na kutoa zawadi kwa wanafunzi waliofaulu, wakuu wa shule za Dini zilizo endesha semina na walimu, hafla hiyo imepambwa na picha zinazo onyesha harakati za Maahadi ya Qur’ani.