Atabatu Abbasiyya tukufu inafanya majlisi kwa watumishi wake ya kuomboleza kifo cha Imamu Baaqir (a.s)

Maoni katika picha
Ndani ya ukumbi wa utawala wa Atabatu Abbasiyya asubuhi ya leo siku ya Alkhamisi, imefanywa majlisi ya kuomboleza kifo cha Imamu wa tano Muhammad Albaaqir (a.s), na kuhudhuriwa na kundi kubwa la watumishi wa Ataba na mazuwaru.

Majlisi imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu, kisha Shekhe Ali Darii akapanda mimbari na kuongea historia ya Imamu (a.s), na matukio ya kihistoria yaliyojiri wakati wa uhai wake (a.s) pamoja na kazi kubwa aliyofanya ya kuonyesha haki na batili.

Hali kadhalika akaongea mambo yaliyotokea wakati wa uhai wa Imamu Baaqir (a.s), likiwepo tukio aliloshuhudia kwa macho yake la mauaji ya Karbala, na yaliyojiri kwa babu yake Imamu Hussein (a.s) na watu wa nyumbani kwake na wafuasi wake.

Akahitimisha kwa kutaja tukio la kifo cha Imamu Baaqir (a.s) kisha akataja tukio la mauaji ya Karbala kihistoria, na waliyofanyiwa watu wa nyumba ya Mtume (a.s), miongoni mwa dhulma ambazo hazijawahi kutokea katika historia.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: