Watumishi wa Ataba mbili tukufu wanaomboleza msiba wa Imamu Baaqir (a.s)

Maoni katika picha
Watumishi wa malalo mbili takatifu ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), wanaomboleza kumbukumbu ya kifo cha nyota ing’aayo Imamu Muhammad bun Ali Albaaqir (a.s).

Siku ya Alkhamisi mwezi saba Dhulhijja maukibu ya waombolezaji wa Ataba mbili takatifu Husseiniyya na Abbasiyya imefanya matembezi ya kuomboleza kutokea ndani ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Watumishi wa malalo tukufu wamekusanyika kuomboleza msiba huo, na kufanya matembezi hadi kwenye malalo ya bwana wa mashahidi (a.s) wakiwa wamejaa huzuni na majonzi makubwa, wakipitia uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu, huku wakiimba kaswida za uombolezaji na kupiga matam.

Matembezi hayo yameishia ndani ya malalo ya Abu Abdillahi Hussein (a.s), ambapo wamepokewa na watumishi wa malalo ya Atabatu Husseiniyya tukufu, ambapo wamefanya majlisi na kusoma mashairi na tenzi za kuomboleza kifo cha Imamu Baaqir (a.s) kwa pamoja.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: