Atabatu Abbasiyya tukufu inajiandaa kupokea mazuwaru wa siku ya Arafa na Iddi

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu imejiandaa kupokea mazuwaru wa siku ya Arafa na Iddul-Adh-ha tukufu, kwa kuweka mkakati wa kuimarisha ulinzi na kutoa huduma za kimazingira na kiafya, inatarajia kupokea idadi kubwa ya mazuwaru.

Makamo katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Mhandisi Abbasi Mussa Ahmadi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Maandalizi ya ziara mwaka huu yameanza mapema, nayo ni ya kwanza baada ya kusimama kwa miaka miwili kwa sababu ya maambukizi ya virusi vya Korona, huduma zimeanza kutolewa mapema na zinaendelea hadi siku ya Arafa ambayo ni siku ya Jumamosi na tutaendelea hadi siku za sikukuu tukufu ya Iddul-Adh-ha”.

Akaongeza kuwa: “Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya umefanya mikutano mingi na vitengo vinavyotoa huduma za moja kwa moja kwa mazuwaru, vilivyo tanguliwa na vikao vya watumishi wa vitengo hivyo, kwa lengo la kutoa huduma bora kwa mazuwaru na kuboresha mazingira”.

Akabainisha kuwa: “Kuna kundi kubwa la watoa huduma wa kujitolea watakaosaidia kazi”, akasema: “Vitengo vyote vya Ataba vimejipanga kuwahudumia mazuwaru watukufu katika siku hizi takatifu”.

Akamaliza kwa kusema: “Kuna mawasiliano endelevu na Atabatu Husseiniyya tukufu pamoja na idara za ulinzi na usalama, Atabatu Abbasiyya inajitahidi kufanya kila iwezalo katika kuhakikisha inatoa huduma bora zaidi kwa mazuwaru”.

Kumbuka kuwa miongoni mwa ziara zinazo hudhuriwa na mamilioni ya watu katika Ataba za Karbala ni ziara ya siku ya Arafa na Iddul-Adh-ha, waumini huja kwa wingi kumzuru Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) na kufanya ziara maalum ya siku ya Arafa na usiku wa Iddi na mchana wake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: