Idara ya teknolojia na taaluma chini ya kitengo cha Habari katika Atabatu Abbasiyya, imeanza kufanya ziara maalum ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) ya siku ya Arafa na usiku wa Idul-Adh-ha tukufu.
Kila anayetaka kufanyiwa ziara na ibada zingine kwa niaba asajili jina lake kupitia link ifuatayo: https://alkafeel.net/zyara/ unaweza kupakua App kwa kutumia simuganja za kisasa kwa link hii: https://alkafeel.net/Apps/Arabic/
Idara imefafanua kuwa ziara hizo zitafanywa na jopo la Masayyid wanaotoa huduma katika Atabatu Abbasiyya tukufu, inajumuisha ibada mbalimbali, kama kusoma dua ya Imamu Hussein (a.s) ya siku ya Arafa, kusoma ziara maalum ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) ndani ya malalo zao takatifu na kuswali rakaa mbili kwa nia ya kukidhiwa haja na kurahisishiwa mambo.
Wataendelea kufanya ibada hadi siku ya Idul-Adh-ha, siku hiyo pia itasomwa ziara ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) pamoja na dua na swala.
Kuna hadithi nyingi zinazo eleza utukufu wa kumzuru Imamu Hussein (a.s) katika siku ya Arafa, kutoka kwa Abu Abdillahi (a.s) anasema: (Atakaemzuru Hussein bun Ali (a.s) siku ya Arafa, Mwenyezi Mungu mtukufu atamuandikia Hijja laki moja pamoja na Qaaimu -a.s- (Imamu Mahadi), na Umra laki moja pamoja na Mtume (s.a.w.w), na ataandikiwa thawabu za kuacha huru watumwa laki moja na kununua katika njia ya Mwenyezi Mungu farasi laki moja, Mwenyezi Mungu atamwita mja wangu rafiki ameamini ahadi yangu, Malaika watasema: Fulani ni muaminifu ametakaswa na Mwenyezi Mungu katika Ashri yake).