Kuhitimisha majlisi za kuomboleza kifo cha Imamu Baaqir na balozi wa babu yake Imamu Hussein (a.s) katika Atabatu Abbasiyya tukufu

Maoni katika picha
Jioni ya Ijumaa ndani ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), imefanywa majlisi ya kuomboleza kifo cha Imamu Baaqir na balozi wa babu yake Imamu Hussein Muslim bun Aqiil (a.s), iliyo ratibiwa na idara ya wahadhiri na Tablighi katika Atabatu Abbasiyya tukufu.

Majlisi hizo zimefanyika kwa muda wa siku nne, tangu siku ya Jumanne, ikiwa ni mihadhara miwili, wa asubuhi unatolewa na Shekhe Ali Darii na jioni siku ya kwanza ulitolewa na Sayyid Muhammad Naqiib na ushiriki wa muimbaji Mustwafa Sudani, na siku tatu zilizobaki mhadhiri alikua ni Shekhe Bilali Alqabisi kwa ushiriki wa muimbaji Ammaar.

Wahadhiri wamezungumza kwa undani tukio hilo la msiba, sambamba na kueleza historia za wahusika.

Kumbuka kuwa majlisi hizi hufanywa kila mwaka chini ya mradi wa Ummul-Banina (a.s), unaohusika na kuandaa maadhimisho mbalimbali yanayo husu Ahlulbait (a.s), ikiwemo kumbukumbu ya kifo cha mjukuu wa Imamu Hussein Imamu Muhammad Albaaqir (a.s) na kifo cha balozi wake Muslim bun Aqiil (a.s), walioaga dunia tarehe tisa mwizi kama huu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: