Idara ya kusimamia haram katika Atabatu Abbasiyya tukufu imeweka utaratibu mzuri wa kufanya ibada za siku ya Arafa.
Wahudumu wa idara hiyo wanaongoza matembezi ya mazuwaru wanao ingia na kutoka ndani ya Haram na kuhakikisha hautokei msongamano.
Hali kadhalika wanawasaidia wazee na watu wenye ulemavu kuwafikisha kwenye haram tukufu na kufanya ziara kwa urahisi.
Kuna jopo maalum la watumishi wa idara hiyo waliosomea utoaji wa huduma ya kwanza na uokozi, wamekaa tayali kutoa msaada wa uokozi wakati wowote utakapo hitajika, Allah atuepushie.
Kazi ya kufanya usafi na kupuliza marashi ndani ya haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s) inafanywa muda wote zaa (24).
Kazi hiyo inafanywa kwa kushirikiana na vitengo vingine vya Atabatu Abbasiyya tukufu.
Kumbuka kuwa idara ya kusimamia haram tukufu katika Atabatu Abbasiyya, hufanya kazi kubwa wakati wa ziara zinazo hudhuriwa na mamilioni ya watu, ikiwemo ziara ya siku ya Arafa na Idul-Adh-ha.