Malalo ya Abu-Abdillahi Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) na uwanja wa katikati ya malalo hizo zinashuhudia kuanza kwa ibada za siku ya Arafa

Maoni katika picha
Muda mfupi kabla ya Adhuhuri siku ya Jumamosi watu wamemiminika kwa wingi katika malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) pamoja na kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili chini ya ulinzi mkali na huduma bora kutoka kwa watumushi wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya kwa ajili ya kufanya ibada za siku ya Arafa.

Watu wamefurika kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili, ndani ya malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), uwanja wa haram ya Aqilah (a.s) na maeneo mengine yote Jirani, watu wengi kutoka ndani na nje ya Iraq huja kufanya Idada za Arafa mmoja mmoja au kwa makundi.

Mazuwaru wameanza kuingia kwa wingi katika eneo hili takatifu toka jana usiku, huanza ibada zao kwa kumzuru Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), kisha husoma dua ya siku ya Arafa ya Imamu Hussein (a.s) sambamba na ibada zingine.

Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa utaratibu maalum wa kuwahudumia mazuwaru hao watukufu na kuhakikisha wanafanya ibada zao kwa amani na utulivu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: