Haram tukufu na uwanja wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) inashuhudia swala ya Idul-Adh-ha

Maoni katika picha
Haram tukufu na uwanja wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) asubuhi ya leo Jumapili, imeshuhudia swala ya Idul-Adh-ha, mazuwaru watukufu wamesimama kwa safu wakiswali swala ya Iddi na kuonyesha unyenyekevu kwa Mwenyezi Mungu.

Baada ya maelfu ya waumini kufurika katika pepo ya Mwenyezi Mungu kwenye ardhi ya Karbala takatifu, katika malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) na kufanya ibada za siku ya Arafa wamehitimisha kwa swala ya Iddi iliyo shuhudia mafuriko ya watu ndani ya haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na maeneo Jirani.

Swala imeswaliwa zaidi ya mara moja kutokana na wingi wa watu, aidha kulikuwa na jamaa kubwa kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu, jamaa hiyo iliongozwa na Mheshimiwa Shekhe Habibu Alkadhimi, huku jamaa nyingine ikiswaliwa ndani ya ukumbi wa haram ya Imamu Hussein (a.s).

Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya tukufu imefanya kila iwezalo katika kupokea mazuwaru wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), na kuhakikisha inawapa huduma bora, huku ulinzi na usalama ukiwa umeimarishwa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: