Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu anapokea watu wanaokuja kutoa pongezi za Idul-Adh-ha

Maoni katika picha
Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Mustwafa Murtadhwa Dhiyaau-Dini asubuhi ya leo siku ya Jumapili akiwa ndani ya ukumbi wa utawala, amepokea viongozi mbalimbali waliokuja kutoa pongezi ya Idul-Adh-ha tukufu.

Miongoni mwa viongozi hao ni mkuu wa mkoa wa Karbala Mhandisi Naswifu Jaasim Alkhatwabi na kamanda mkuu wa mkoa, wamepeana pongezi ya sikukuu tukufu.

Aidha amepokea viongozi wa idara, marais wa vitengo na wahutumu wa malalo ya Abulfadhil Abbasi waliofika kumpa mkono wa Idul-Adh-ha, na kumuomba Mwenyezi Mungu airudishe siku hii tena mwakani tukiwa salama.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: