Zaidi ya watu laki moja wamefanyiwa ziara ya Arafa na Iddi kwa niaba

Maoni katika picha
Idara ya teknolojia na taaluma za mitandao chini ya kitengocha Habari katika Atabatu Abbasiyya imesema kuwa zaidi ya watu (103,732) wamefanyiwa ziara ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) katika usiku wa Arafa, mchana wake na usiku wa Iddi na mchana wake ndani ya malalo zao tukufu, kupitia mtanda wa Alkafeel (toghuti rasmi ya Atabatu Abbasiyya tukufu) na App zake za kwenye simu ganja za kisasa.

Sayyid Haidari Twalibu Abdul-Amiir akafafanua kuwa “Ziara ya Arafa na Iddi ni miongoni mwa ziara muhimu huwa na ratiba maalum, ambayo hutekelezwa na Masayyd wanaotoa huduma katika Atabatu Abbasiyya tukufu, huanza usiku wa Arafa hadi siku ya kwanza katika sikukuu ya Idul-Adh-ha”.

Akaongeza kuwa: “Ibada walizofanya ni pamoja na ziara ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) katika usiku wa Arafa, mchana wake, usiku wa Iddi na mchana wake, na swala ya rakaa mbili mbele ya malalo zao takatifu sambamba na ibada za mchana wa Arafa kama vile dua na zinginezo”.

Sayyid Mamitha Akabainisha kuwa: “Maombi ya kufanyiwa ziara yametumwa kupitia dirisha la ziara kwa niaba kwenye mtandao wa kimataifa Alkafeel, kwa lugha zake zote (Kiarabu – Kiengereza – Kifarsi – Kituruki – Kiurdu – Kifaransa – Kiswahili – Kijerumani), maombi yametoka kwenye mataifa tofaoti ya kiarabu na kiajemi bila kusahau taifa la Iraq”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: