Makumi ya mabinti wamehitimu semina ya pili ya (Yanabiia Rahmah)

Maoni katika picha
Idara ya Qur’ani chini ya ofisi ya maelekezo ya Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu imekamilisha ratiba ya semina ya pili ya (Yanabiia Rahmah), ambayo wameshiriki makumi ya mabinti wenye umri wa miaka (10 – 11 – 12).

Kiongozi wa idara bibi Fatuma Mussawi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Hakika semina ya pili ni muendelezo wa semina ya kwanza, masomo yanaendana na umri wa washiriki, nao ni wanafunzi wa mkoa mtukufu wa Karbala, semina imedumu kwa muda wa siku kumi na tano, ilikua na vipengele vingi vinavyo lenga kuwajenga na kuwaongezea maarifa katika masomo ya Dini”.

Akaongeza kuwa: “Ratiba ya masomo pia ni muendelezo wa ratiba ya awali, wamefundishwa usomaji sahihi wa Qur’ani, hukumu za usomaji, udhu, swala, Aqida, aidha wameonyeshwa filamu ya historia ya Maimamu wa Ahlulbait (a.s) sambamba na kuweka mdahalo huru na kujibu maswali”.

Akafafanua kuwa: “Mwisho wa semina vimetolewa vyeti vya ushiriki vyenye nembo ya Atabatu Abbasiyya tukufu sambamba na maneno mazuri ya pongezi, wazazi na walezi wa washiriki wameshukuru sana na wakaomba semina iendelee siku zijazo kutokana na umuhimu wake”.

Kumbuka kuwa hii ni moja ya semina nyingi zinazo fanywa na idara yetu, imefanywa baada ya kukamilisha maandalizi yote, ikiwa ni pamoja na selebasi ya masomo, usafiri wa kwenda na kurudi, zawadi kwa washindi na vyeti vya ushiriki.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: