Wanafunzi wa Dini wamehitumu semina ya Qur’ani

Maoni katika picha
Idara ya hauza katika Maahadi ya Qur’ani tukufu mjini Najafu chini ya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya, imekamilisha semina ya pili katika mradi wa Qur’ani kwa wanafunzi wa hauza.

Kiongozi wa maswala ya hauza katika Maahadi Shekhe Mahadi Bayati amesema: “Semina ilikua na wahadhiri kutoka hauza na makhatibu wa mimbari ya Husseiniyya, wamefundisha masomo yanayohusu maarifa ya Qur’ani”.

Akaongeza kuwa: “Mihadhara miwili ilihusu umuhimu wa kujifunza Qur’ani tukufu hasa kwa wanafunzi wa Dini, na kusisitita kuhusu miujiza ya Qur’ani sambamba na kuzingatia maudhui za Qur’ani zinazo eleweka kwa kila mtu, wakasema kuwa jukumu la mwalimu wa Qur’ani ni kufafanua maudhui hizo kwa wanafunzi na watu wote kwa ujumla”.

Akabainisha kuwa: “Miongoni mwa wahadhiri ni (Dokta Muhammad Zawiin mwalimu wa mfumo wa masomo – Dokta Ni’mah Asadi mwalimu wa mbinu za ufundishaji – Shekhe Baasim Aabidi mwalimu wa mifumo ya tafsiri na wafasiri – Shekhe Karim Masira mwalimu – Ustadh Ahmadi Salim mwalimu wa hukumu za usomaji na uandishi wa Qur’ani – Pamoja na mkaribishaji wa watoa mada, fani za Qur’ani zinautaratibu wake)”.

Akafafanua kuwa: “Maahadi ilikaribisha viongozi wa hauza, miongoni mwao ni Hoja ya Uislamu Sayyid Izudini, Mheshimiwa Shekhe Ghazwani Alkhuzai, Mhadhiri wa Husseiniyya Sayyid Jafari Muruji, kwa ajili ya kukazia maarifa”.

Kumbuka kuwa semina imedumu kwa muda wa siku kumi na mbili, muda wa masomo ulikua saa sita kila siku, jumla ya wanafunzi walikua arubaini waliochaguliwa kutoka wanafunzi zaidi ya mia tano walio shiriki kwenye mradi wa Qur’ani kwa wanafunzi wa Dini awamu ya kwanza na ya pili, baada ya semina hii wanakua walimu bobezi katika masomo ya Qur’ani na baada ya kufanya mitihani ya nadhariyya na vitendo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: