Shule za Al-Amee ambazo ziko chini ya kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimefaulisha kwa kiwango cha juu kabisa (%100) kwenye matokeo ya mtihani wa wizara katika mkoa wa Karbala kwa mwaka wa masomo (2021 – 2022m), zimeingizwa kwenye orodha ya shule bora zaidi.
Mafanikio haya ni muendelezo wa mafanikio yaliyotangulia, kiwango cha ufaulu katika shule ya sekondari Al-Ameed ya wasichana na Nurul-Abbasi “a.s” ya wasichana pia ni (%100), huku sekondari ya Bwana wa maji ya wavulana ikifaulu kwa asilimia (%98.95), na sekondari ya Alqamaru ya wasichana ikifaulu kwa (%97.8).
Kitengo kinawapongeza wazazi na walezi wa wanafunzi kwa ufaulu huo mkubwa uliopatikana, sambamba na kupongeza idara za shule na walimu kwa kazi nzuri waliyofanya hadi kupata mafanikio hayo, kwani kufanya kazi kwa juhudi ndiko huleta mafanikio.