Kufanyika kwa nadwa ya wanawake inayohusu sekta ya Tablighi kujiandaa na mwezi wa Muharam

Maoni katika picha
Kitengo cha kuandaa mubalighaat katika chuo kikuu cha Ummul-Banina (a.s) chini ya kitengo cha elimu na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimeandaa nadwa ya wanawake inayohusu sekta ya Tablighi, nadwa hiyo imepewa jina la (Nafasi ya Mubalighah… fursa na changamoto) kwa ajili ya kujiandaa na mwezi mtukufu wa Muharam.

Rais wa chuo Shekhe Hassan Turabi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Hakika nadwa imefanywa kwa njia ya mtandao kupitia jukwaa la mawasiliano ya kijamii kwa ajili ya kujiandaa na mwezi mtukufu wa Muharam, nadwa hii inalenga kunoa vipaji vya uongeaji kwa washiriki na kuwafanya waweze kufikisha sauti ya harakati ya Imamu Hussein kwa njia za kisasa”.

Akaongeza kuwa: “Mhadhiri wa nadwa hiyo alikua ni mwalimu mbobezi wa Tablighi, ameongea kuhusu umuhimu wa nafasi ya mubalighah wa leo, na kufanyia kazi usia na maelekezo ya Marjaa Dini mkuu kwa mubalighina, pamoja na umuhimu wa kunufaika na fursa za Tablighi, na maendeleo yanayoshuhudiwa kwenye sekta hiyo, hali kadhalika changamoto anazokutana nazo mubalighah wa leo na namna ya kuzishinda”.

Akabainisha kuwa: “Ameongea pia kuhusu njia za kisasa za kuwasilisha ujumbe wa Imamu Hussein, kwa kutumia dalili za kielimu na hadithi za Mtume na Ahlulbait (a.s)”.

Akamaliza kwa kusema: “Nadwa imeshuhudia muitikio mkubwa kutoka kwa washiriki, wametoa maoni yao na kuuliza maswali, naye mtoa mada amejibu maswali na kutoa ufafanuzi zaidi pale ulipohitajika”.

Kumbuka kuwa chuo kikuu cha Ummul-Banina (a.s) kwa njia ya mtandao, kinaendelea kufanya nadwa na kutoa mihadhara ya kielimu, kwa lengo la kujenga uwezo wa wanafunzi wake, na kuimarisha sekta ya elimu na Tablighi kwenye sekta mbalimbali za Dini.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: